Picha ya msanii Belle 9
Akizunguzmzia hilo kwenye show ya Planet Bongo ya East Africa Radio, Belle 9 mwenyewe amesema ameamua kuiita EP yake Boss Baba kwa sababu mtoto wake wa kwanza anaitwa Boss, hivyo watu humuita Baba Boss.
"Nimeiita EP yangu 'Baba Boss' kwa sababu nilitaka watu wajiulize maswali lakini pia mimi ni Baba Boss, Mtoto wangu wa kwanza anaitwa Boss hiyo ndio sababu ya kuiita EP yangu hivyo" ameeleza Belle 9





