Jumatatu , 15th Jun , 2015

Mwanamuziki wa R&B Steve R&B ameelezea sababu zilizomfanya kukaa kimya kwa muda mrefu na kushindwa kutoa kazi yoyote.

Steve R&B

Star wa muziki Steve R&B ameeleza kuwa, safari zake nyingi za kimuziki nje ya nchi zimekuwa ndio sababu ya yeye kupunguza kasi ya projekti zake binafsi hapa nchini, akiwa sasa katika mpango wa kuweka ratiba zake sawa ili kuwatendea haki mashabiki zake, familia na sanaa yake.

Staa huyo amesema kuwa, anafahamu dhahiri kuwa kuna kitu kimekosekana kwa muda kwa upande wa sanaa yake kama msanii binafsi, akiwa sasa analifanyia hilo kazi ili kurekebisha hali ya mambo kama anavyoeleza mwenyewe hapa.