Sakata la hela za rambirambi, Wakazi aibuka

Ijumaa , 22nd Feb , 2019

Sakata la kuibwa kwa pesa za rambi rambi za msiba wa msanii Godzilla, limemuibua rapper Wakazi ambaye alikuwa ni mmoja ya wakusanyaji wa michango hiyo, ambayo inalalamikiwa kuibwa na watu wengine.

Kwenye ukurasa wake wa twitter Wakazi ameandika ujumbe akisema kwamba alijua suala hilo tangu wakati wa msiba, lakini alishindwa kuliweka wazi kwani hakuwa kwenye nafasi ya kulizungumzia.
 

Wakazi alienda mbali zaidi kwa kuzungumzia suala la Fid Q kuweka wazi kilichotokea, na kueleza kuwa huenda Fid Q alishindwa kukaa nalo moyoni lakini hakustahili kulizungumzia, bali angewaachia wana familia.