Ijumaa , 30th Mei , 2014

Katika jitihada za kurasimisha kazi za sanaa hapa Tanzania na pia kuhakikisha wasanii wanafaidi kupitia kazi zao za sanaa, hususan katika upande wa muziki na filamu, Serikali ya Tanzania imetangaza kuanza kwa mchakato wa kuziondoa kazi feki za sanaa.

Katika maelezo yake jana alasiri bungeni, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amesema kuwa, tayari Serikali imekwishatoa stika zaidi ya 6,000 kwa ajili ya kazi halali za wasanii, na kutoa muda wa kutosha kwa wale ambao wana kazi zilizo nje ya utaratibu huu kuziondoa sokoni ambapo sasa wakati umekwishafika kwa serikali kuingilia kati.