Ijumaa , 22nd Jul , 2016

Jaji wa miaka mitano tangu shindano la Dance100 lilipoanza mwaka 2012 Super Nyamwela amesema shindano la Dance100 linalipa sana kwa washiriki kwa sababu wengi baada ya ushiriki wameweza kuchukuliwa na bendi mbalimbali pamoja na wasanii binafsi.

Jaji wa Dance100 Super Nyamwela

Super Nyamwela ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na EATV kuhusu mafanikio ambayo mshiriki anaweza kuyapata kwa kushiriki shindano hilo.

‘’Tangu Dance100 ilipoanza mwaka 2012 vijana wengi wameweza kupata ajira katika bendi mbalimbali na kutambulika na jamii kupitia vipaji vyao, wengine wametoka hadi nje ya nchi hivyo ni vyema wazazi na jamii wakathamini kazi ya uchezaji kama kazi nyingine halali’’ Amesema Jaji Super Nyamwela

Jaji huyo ameongeza kwamba Kuwa ‘dancer ‘ siyo uhuni bali ni kazi kama kazi nyingine ambayo inatoa kipato kwa watu kuweza kupata kipato na maendeleo.

Aidha amewataka washiriki wa shindano hilo kuwa wamoja na kuongeza juhudi na kuhakikisha wanakuwa wabunifu ili kuonyesha utofauti wa mwaka huu na mwaka jana.

Shindano la Dance100 linaendelea kesho katika nafasi ya pili ya usaili ambapo usaili unafanyika viwanja vya Don Bosco Upanga kuanzia saa nne asubuhi na kuonyeshwa siku ya Jumapili saa moja usiku.

Tags: