
Q Chief ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba directors wa ndani hawana lolote, hivyo ataenda kufanya kazi zake nje.
"Kama nina accesess ya kutoka nje na kufanya mambo yangu ya maendeleo sina haja ya kustick na watu wa bongo, i've been here for ten years, kama hukuona kitu nyuma, huwezi kuona kitu sasa.
Chillah ameendelea kusema "Sio kama nawatukana, lakini naona directors ambao wanajitanua wakati bado, we ukivimba Moe Musa afanye nini, mtoto mdogo wewe hujamfikia hata Tedy Josiah Kenya, nyie bado mna changamoto alafu hili mtalielewa, si tunapanda ndege tunaenda kushutia mbali tukirudi tunaachia vyuma, mkijipanga kitabia, mkijipanga kimaisha kimaendeleo production wise, we will come alafu mtataja bei zenu milioni 17 tutalipa tutashoot", alisema Q Chillah.
Pia Q Chief amewataka directors wa ndani wajifunze zaidi na kuacha tamaa ya kutaka malipo makubwa toka kwa wasanii, kwani wanaharibu ndoto za wasanii.
"Hawa waliokuwepo their brain has stuck, wamekwama, yani hawa wamekwama kuliko mimi, kina Hanscana sijui nani, these kids they need to learn more, you need to believe dream ya msanii, msanii ana dream yake unamtajia milioni 17 wakati wewe mwenyewe unataka kuondoka, huoni kama ujinga huo, mi siwezi kuentertain hivyo vitu, napanda ndege naenda kushoot mbele naleta mjini", alisema Q Chief.