
Picha ya msanii Gelly Wa Rhymes
Gelly wa Rhymes amesema sasa hivi hafanyi tena dhambi, kwa sababu kipindi cha nyuma alishatenda dhambi nyingi kupitia tendo hilo, ambalo alikuwa anafanya pasipo kuoa mwanamke yeyote.
"Kinachoendelea kwa sasa hivi ni furaha tu, nai-enjoy kuwa na mwanamke anayenielewa, mnyamwezi, anasapoti kazi zako, mpambanaji na haingiliani na unachokifanya halafu nafurahia sasa hivi tendo la ndoa nalifanya kihalali sio dhambi, maana mwanzo nilitenda dhambi nyingi" ameeleza Gelly Wa Rhymes.
Pia msanii huyo ameendelea kusema "Halafu unaambiwa ukioa kiislamu unafutiwa dhambi zako zote unaanza na moja, kwa hiyo nafurahi kufanya hivyo kihaki kabisa unajua mpaka nimefikia kuoa nimefanya hivyo mara nyingi bila uhalali, kwa sababu ya ujana tu ila sasa hivi nimeamua kwenda huku kidogo".