''Sijawahi kuwa single'' - Dogo Janja

Jumatano , 10th Jul , 2019

Msanii wa kizazi kipya kutokea Arusha Dogo Janja "Janjaro", amefunguka kuwa anajipanga kuoa tena na amesema hajawahi kuwa single katika maisha yake tangu ayajue mapenzi.

Dodo Janja

Dogo Janja amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, baada ya kuwapa ruhusa mashabiki zake kuuliza maswali wanayotaka ili awajibu.

Janjaro amejibu mengi ikiwemo maisha yake na kazi za muziki, mahusiano na maisha ya shule. Baadhi ya majibu aliyotoa msanii huyo baada ya kuulizwa maswali hayo alisema kuwa, 

"Kuoa ni jambo la kheri nikijipanga inshaalah, sijawahi kuwa single katika maisha yangu toka niyajue mapenzi, mi huwa sifanyi kazi kwa mazoea, na wasanii ninaowakubali ni Aslay, Bob Marley na Muhogo Mchungu pia anatamani kufanya kazi na Chris Brown."