
Gigy Money
Akizungumzia kuhusu tukio lake la kwenda kanisani, ambalo liliwachanganya watu wengi hasa baada ya ku'post' picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram Gigy Money amesema, watu wasimkariri kwenye maisha haya.
"Acheni kunikariri jamani msifanye mnanijua sana, kwa hiyo hapo kanisani mnataka aende nani nisingeenda mnasema nimeenda mnasema, ila mimi nafanya imani yangu inavyotaka nifanye, kwenda kanisani ni mtu yeyote anaenda kwa anayetambua wajibu wake kama binadamu" amesema Gigy Money.
"Kanisani naenda sio kwamba mimi ni mlokole ambaye nashinda kanisani, naenda kumuomba mungu pale napota nafasi mimi ni Mama, msanii na kioo cha jamii labda nikionekana kuna muda naonekana natafuta kiki" ameongeza
Aidha Gigy Money amegusia suala la kutokwa na damu nyingi, kipindi akiwa katika siku zake kama mwanamke.
"Nilikuwa nasumbuliwa sana nikiwa katika "Period" zangu na nilikuwa nikivaa pedi damu yangu nyingi ilikuwa inatoka nje, hedhi yangu ilikuwa inaonekana nilikuwa nadhalilika, ni changamoto iliyonikuta wakati nasoma shule na nilitamani iwe likizo likinikuta tatizo hilo" ameeleza.