Jumamosi , 1st Feb , 2020

Producer Mr T-Touch ameuingilia ugomvi wa msanii Alikiba na producer wake wa zamani Man Water, juu ya tofauti zao ambazo zinaendelea kwa sasa za kudaiana pesa na kufutiana nyimbo.

Kutokea upande wa kushoto ni Mr T-Touch, Alikiba na Man Water

Akitoa maoni yake kupitia EATV & EA Radio Digital, Mr T-Touch amesema, linapotokea suala kama hilo huenda likamuathiri mmoja wapo, ila itategemeana na utendaji kazi wao na kila mtu ana haki yake.

"Msanii na producer wanategemeana kwenye kazi mwisho wa siku kila mtu anabiashara yake, kwa upande wa Man Water kama alikuwa hajalipwa kweli ni haki yake kulipwa, na nilivyosikia mimi ni kwamba wameshindwana kulipana na Alikiba ameenda kuzirudia nyimbo sehemu nyingine" amesema Mr T-Touch.

Aidha ameongeza kusema, "Kulikuwa na biashara kichaa na ushkaji ndani yake ambao umeafanyika halafu kila mtu anamlaumu mwenziye, pia itategemea na makubaliano ambayo wamejiwekea kwa mimi upande wangu mara nyingi kama kazi ya kulipana basi tulipane hapo hapo ili ikitokea tumetofautiana tayari nimeshachukua pesa yangu".