Tausi afungukia kuhusu kutoa mimba

Jumatano , 14th Feb , 2018

Msanii wa filamu nchini Tanzania na kipenzi cha watoto, Tausi Mdegela amefunguka na kudai hajawahi kutoa ujauzito wowote mpaka sasa wala kushika mimba japokuwa anatamani siku moja na yeye kuwa na familia yake.

Tausi ametoa kauli hiyo kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kwenye ukurasa wa facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mchana mpaka saa 10 alasiri wakati alipokuwa anajibu swali lililoulizwa na muongoza kipindi hicho aliyetaka kufahamu kwamba msanii huyo alishawahi kutoa mimba.

"Sijawahi kutoa ujauzito na wala sijawahi kushika kabisa mpaka sasa. Natamani siku moja nami niwe na familia yangu. Huwa siangalii sana umri kwenye suala la mahusiano hata kama ana miaka 18 ili mradi awe na future katika mahusiano yetu", amesema Tausi.

Kwa upande mwingine, Tausi amesema anazidi kupambana katika kazi zake ili siku moja nae aje kuendesha ndege.

Lipa kwa M-PESA sasa na upate zawadi na punguzo katika sehemu mbalimbali za huduma kwa kubonyeza *150*00# au MENYU ya mtandao uliopo, VODACOM, PESA NI M-PESA.