Jumamosi , 14th Mar , 2015

Star wa muziki Mheshimiwa Temba amezungumzia suala la yeye kubadilika na pia kubadili muziki wake kutokana na ngazi aliyofikia, ambapo amesema kuwa kwa upande wake hawezi kuishi maisha ya kuigiza ambapo atakuwa anaidanganya jamii.

Mhe. Temba

Star huyo ambaye hivi karibuni amekanusha ripoti zilizokuwa zimesambaa kuhusu yeye kuhusika katika kesi ya kutishia maisha, amesema kuwa chochote anachofanya na kile alichonacho ndicho ambacho kitaonekana na watu kutoka kwake na si zaidi.

Temba ambaye amedumu katika game ya muziki toka mwaka 1994, amesema kuwa kile anachokifanya ndicho kilichomfikisha alipo sasa, na kukibadilisha kutamfanya kujidanganga na kuidanganya jamii inayomzunguka.