Tessy afunguka kutafutiwa madanga na Uwoya

Ijumaa , 11th Jan , 2019

Mzazi mwenzake msanii Aslay, Tessy Chocolate, ameweka wazi juu ya tuhuma zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa Irene Uwoya anamtafutia wanaume, kutokana na ukaribu waliokuwa nao.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Tessy amesema kwamba ukaribu wake na Uwoya ni upendo tu uliopo baina yao, na pia humpa ushauri wa mambo mbali mbali ya maisha na sio mahusiano tu.

“Ni upendo tu tuliokuwa nao, tunaheshimiana, tunafanya vitu vingi, tunashauriana vitu vingi vya kimaendeleo, ukiacha mahusiano, mahusiano ni vitu private, hasa hasa ni katika maendeleo kwa sababu hapendi kuona anguko langu, yeye ni mkubwa kwangu amenizidi miaka mingi hivyo hunishauri”, amesema Tessy.

Hivi karibuni baadhi ya watu mitandaoni wamedai kwamba ukaribu uliopo baina ya wawili hao hasa baada ya Tessy kuachana na Aslay, ni kutafutiana wanaume, kwani wawili hao hawafanani kiumri kiasi cha kuwa marafiki.