Alhamisi , 31st Dec , 2020

2. Shilole kupigwa na Uchebe
Ilikuwa siku ya Julai 8, 2020 ambapo msanii na mfanyabiashara Shilole kuandika mazito ambayo amekutana nayo kwenye ndoa yake na aliyekuwa mume wake Uchebe, kwenye taarifa yake hiyo aliyoweka kwenye mtandao wa Instagram ameeleza kuwa amekutana na ukatili

Kushoto ni tukio la Shilole kupigwa na Uchebe, kulia ni Kiki ya kifo ya msanii wa singeli Meja Kunta.

wa kupigwa hadi kuumizwa na Uchebe pia ndiyo siku aliyotangaza kuachana na mwanume huyo.

Wasanii, viongozi, mashabiki na taasisi za kijamii zilikemea vikali tukio hilo huku wakitaka Uchebe kuchukuliwa hatua kali za kisheria baada ya kufanya tukio hilo, kesi ilifika mbali zaidi hadi kupeana talaka na kufikishana Mahakamani.

3. Kiki ya Kifo ya Meja Kunta

Mapema kabisa siku ya Februari 1, zilitoka taarifa kwamba msanii wa singeli Meja Kunta amepata ajali ya gari maeneo ya Segera wakati anatoka Dar Es Salaam kwenda kufanya show Mkoani Tanga, hivyo amekimbizwa Hospitali ya Mkwakwani.

Siku moja baadaye meneja wake alitoa taarifa kwenye mtandao wa Instagram kwamba msanii huyo amefariki dunia, kumbe tukio hilo lilikuwa limetengenezwa kwa ajili ya kiki ya kumsogeza mahali msanii huyo, baadaye uongozi mzima wa lebo yake na Meja Kunta mwenyewe waliomba radhi kwa Watanzania kwa tukio hilo.

4. Mzee Yussuf kurudi kwenye muziki baada ya miaka mitano 

Tukio namba 4 kwenye yale matukio yaliyotikisa kwenye burudani mwaka 2020 basi ilikuwa ni 'comeback' ya msanii wa Taarab Mzee Yussuf baada ya kupita miaka mitano tangu alipotangaza kuacha kufanya muziki na kuhamia kwenye Ibada.

Madeni kutoka Benki na Nyumba kutaka kupigwa mnada ndiyo sababu inayodaiwa Mzee Yusuph kurudi tena kwenye Taarab, pia mwenyewe aliongeza kusema amerudi kwa sababu watu walim-miss na pengo lake lilishindwa kuzibika.

5. Killy na Cheed kutoka kwa Alikiba kwenda kwa Harmonize

Tukio la 5 lililo'trend sana 2020 ni siku ya Aprili 13 ambapo wasanii Cheed na Killy walitangaza ku-left kwenye lebo ya Kings Music Records ya Alikiba na baadaye wakaenda kumwaga wino Konde Gang Music ya Harmonize, tukio hilo lilishangaza wengi kwani halikutarajiwa kwani Alikiba ndiyo aligundua vipaji vya wasanii hao na kuwapa sapoti ya kuwasimamia kwenye kazi zao.

6. Wema kubadilisha muonekano wake 

Ile 'Round up' ya matukio ya burudani yaliyo'trend sana mwaka inahitimishwa kwa muonekano mpya wa staa wa filamu Wema Sepetu ambaye inasemekana amefanya 'surgery' ya kukata utumbo ili kuweza kupunguza shepu ya umbile lake.

Baada ya kufanya kitendo hicho Wema Sepetu amebadilika sana na ameonekana kupungua kinoma noma na ubaya zaidi huwa anazungumziwa na kushambuliwa kila siku anaposhea picha mpya kwenye mitandao ya kijamii na watu kumzingua kwamba amepoteza mvuto.