Jumatatu , 16th Aug , 2021

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa amesema Wizara yake imerudisha tuzo za muziki na sanaa mbalimbali ambazo zitafanyika mwishoni mwa mwaka huu 2021.

Picha ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Innocent Bashungwa akiwa kwenye kipindi cha DADAZ

Waziri Bashungwa amezungumza hilo kupitia show ya DADAZ ya East Africa TV ambapo amesema

"Tumerudisha tuzo za kila mwaka na mwaka huu mwishoni tutakuwa na tuzo na mambo mengi yaliyokuwa na faida huko nyuma chini ya uongozi wa Rais Samia tunayarudisha, tuzo za muziki na sanaa mbalimbali vyote vinarudi".

Zaidi tazama hapa akizungumzia hilo.