Alikiba alivyosherehekea Birthday yake Tabora

Ijumaa , 29th Nov , 2019

Msanii wa Bongoflava Alikiba ambaye leo ni siku yake ya kuzaliwa, amesherehekea na wanafunzi wa Chuo cha Uhazili Tabora ambapo amewakumbusha kutumia vipaji vyao pamoja na Elimu kutimiza ndoto zao.

Msanii wa Bongoflava Alikiba.

Akiongea na wanafunzi hao Alikiba ameeleza kufurahishwa na mapokezi aliyopata, ambapo katika kueleza historia yake akawataka wafuate nyayo zake ambazo ni kuzingatia elimu, kipaji na kuwa na nidhamu.

'Mimi pia nilikuwa kama nyie, niligundua kipaji changu cha kuimba nikiwa shule nikaendelea na Elimu na kuimba pia huku nikiwa na nidhamu na watu wote ninaofanya nao kazi ni leo ni matokeo ya kipaji changu hivyo na nyie someni lakini mtazame vipaji pia ili muweze kuajiri wengine', amesema Alikiba.

Msanii huyo ambaye anatimiza miaka 17 kwenye muziki anatarajia kufanya tamasha Kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi likifahamika kama #AlikibaUnforgettableTour ambalo linapewa nguvu na East Africa Television pamoja na East Africa Radio.