Alhamisi , 1st Jun , 2017

Muigizaaji na Mwimbaji, Snura Mushi mwenye 'hit' ya 'Nionee wivu' amewmafanikio aliyonayo sasa ni kutokana na juhudi zake binafsi za upambanaji pasipo kumtegemea mwanaume yoyote kwenye maisha yake.

Msanii Snura Mushi

Snura amebainisha hayo hivi karibuni alipokuwa akieleza ni namna ganii aliweza kupambana hadi kufikia alipo leo, huku akifafanua kwamba  baadhi ya watu kuwa na dhana iliyojengeka katika akili zao kuwa kila mwanamke mwenye mafanikio ya aina yoyote lazima atakuwa ameyapata kutoka kwa wanaume aliotembea nao kimapenzi.

"Nilishalala njaa sana tu, tena wakati natoka kwa wazazi na kuanza maisha yangu binafsi ya kujitegemea, nilikuwa na wakati mgumu sana nakumbuka nilikuwa nashindia ugali na mbilimbi na nilikuwa jeuri sana japo nilikuwa na shida zangu kwa sababu maisha hayo hayakufanya nimtegemee mwanaume" alisema Snura