Ulevi, ugomvi na mama yake vimefanya kuacha muziki

Jumanne , 23rd Jun , 2020

Msanii Vanessa Mdee amesema hataki kuwa sehemu ya tasnia ya muziki na mfumo wa kazi wala kwenye soko la muziki, pia amehusisha sababu kama ulevi uliopitiliza, ugomvi na mama yake,sapoti huzuni na presha ndiyo vimemfanya kuacha muziki

Vanessa Mdee

Akifafanua suala hilo la kuacha muziki kupitia YouTube Channel yake Vanessa Mdee amesema 

"Nimepitia changamoto nyingi sana kwenye upande wa muziki na imenipelekea kutaka kuacha au kuamua kuacha kuwa sehemu ya soko la muziki, nyuma ya pazia tasnia ya muziki ni tasnia ambayo bila ya kufahamu au kuielewa vizuri unaweza ukaona tunafanya show, tunasafiri, tunaachia nyimbo tuna mashabiki lakini kiukweli sio sehemu ya kawaida ya maisha ya mwanadamu

Pia kupitia Podcast yake inayoruka mtandaoni Vanessa Mdee amesema alikuwa na ugomvi na mama yake kuhusu muziki hali iliyokuwa akikosa sapoti kutoka kwa mzazi wake huyo, pia ulevi, huzuni na presha vimechangia kuacha muziki.