Undani kifo cha mwanamuziki Aurlus Mabélé

Ijumaa , 20th Mar , 2020

Staa na nguli wa muziki wa Soukous kutoka DR Congo, Aurlus Mabélé amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 67. Chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi lakini Mabélé alikuwa akisumbuliwa na Saratani (cancer) kwa muda mrefu.

Marehemu Aurlus Mabélé

Kwa mujibu wa mwanamuziki Nyboma Mwandido, Mabele amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali moja jijini Paris Ufaransa.

Nyboma amesema Mabele alilazwa hospitalini Alhamis Machi 19, 2020 usiku.

Sababu rasmi ya kifo chake bado haijawekwa wazi huku vyanzo mbalimbali vikieleza huenda ni Corona na vingine vikisema ni mshtuko.