Jumapili , 17th Jul , 2016

Baada ya usaili wa awamu ya kwanza kuanza kwa mafanikio makubwa kwa makundi matano kuchaguliwa katika viwanja vya Leaders Jijini Dar es salaam , usaili wa pili kufanyika Jumamosi tarehe 23 Julai 2016 Viwanja vya Don Bosco Upanga Jijini Dar es salaam.

Mtangazaji wa Shindano la Dance100% Tbway 360 alipokuwa akiendelea na kazi viwanja vya Leaders Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mmoja wa waratibu wa shindano hilo Brendansia Kileo kutoka EATV, usaili wa Jumamosi ijayo utatafuta makundi mengine matano ambapo makundi yote pamoja na matano yaliyofuzu katika usaili wa awali yatasubiri usaili wa mwisho tarehe 30 Julai ndipo hatua ya robo fainali ianze.

Zawadi kwa msimu huu kwa mshindi imeongezeka kutoka shilingi milioni tano hadi saba ambapo shindano hilo linadhaminiwa na Kampuni ya Vodacom pamoja na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola.

Aidha usaili wa mashindano haya ni bure hivyo vijana wametakiwa kujitokeza kwa wingi ili kuonesha vipaji vyao na kunufaika na zawadi itakayotolewa.
Sambamba na zawadi hiyo, shindano hilo litakuwa linarushwa kila siku ya Jumapili saa moja usiku.

Tags: