Alhamisi , 6th Aug , 2015

Usaili wa tatu na wa mwisho wa mashindano makubwa kabisa ya kudansi nchini Dance 100% 2015, unakamilika Jumamosi hii kwa kishindo kikubwa katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni.

mashindano makubwa ya kudansi nchini Tanzania Dance 100% 2015

Hii inakuwa ni nafasi ya mwisho kuingizwa kwa makundi yatakayopambana katika mashindano hayo kwa mwaka huu.

Katika usahili huo makundi mengine makali yatasakwa kuungana na makundi 10 ambayo tayari yamefanikiwa kuingia katika mpambano, tukio ambalo litaandamana na burudani mbalimbali, ushindani ukitarajiwa kuwa mkubwa zaidi kutokana na makundi kuendelea kujinoa zaidi kuridhisha majaji.

Tukutane Jumamosi, shughuli itaanza saa 4 mpaka saa 10 jioni, kwa makundi muhimu ni kuwahi zaidi na kumbuka, burudani hii yote haina kiingilio.

Fuatilia pia yaliyojiri katika usahili ulipita wa mashindano hayo kupitia shoo kali ya Dance 100% 2015, siku ya jumamosi, kuanzia saa 12:30 jioni, hapa EATV pekee.