Jumamosi , 23rd Jul , 2016

Baada ya kumaliza usaili wa pili kwa mafanikio makubwa kwa mashindano ya Dance100 2016 katika viwanja vya Don Bosco Upanga, usaili wa mwisho utafanyika viwanja vya TCC Chang'ombe Jijini Dar es salaam tarehe 30. 07.2016

Kundi la J Combat Crew kutoka Zanzibar lilipokuwa likionyesha vipaji katika uwanja wa Don Bosco Upanga Dar es salaam

Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo Bhoke Egina usaili wa Chang’ombe utakuwa ni wa mwisho ili kupisha hatua ya robo fainali, nusu fainali na fainali yenyewe kwa watakaofanikiwa kusonga mbele.

‘’Usaili wa tarehe 30 utakuwa ni usaili wa mwisho ambapo makundi matano yatachaguliwa katika usaili huo na baada ya hapo yataungana na makundi mengine yaliyoshinda usaili wa kwanza na wa pili ili kutafuta watakaofuzu hatua ya robo fainali’’ Amesema Bhoke Egina

Dance100% inarushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumapili saa moja jioni chini ya udhamini wa Vodacom na Coca-Cola.

Tags: