Ijumaa , 29th Jul , 2016

Shindano la Dance100% linaloendeshwa na kituo cha EATV litaendelea kesho katika viwanja vya TCC Chang'ombe ambapo kesho tarehe 30 Julai 2016 ni usaili wa mwisho kabla ya kuanza kwa mchuano wa robo fainali.

Kundi la Mafya Crew ambalo lilishiriki usaili wa kwanza.

Akizungumzia shindano la kesho mratibu Bhoke Egina amesema shindano la kesho litakuwa babu kubwa kutokana na washiriki kutambua kwamba ni usaili wa mwisho hivyo ni shindano ambalo litakuwa la aina yake katika usaili wa msimu huu.

''Kesho ni usaili wa mwisho na ikumbukwe kwamba kutokana na zawadi ya mwaka huu kuongezeka hadi kufikia milioni 7 kumefanya hamasa kubwa sana hivyo watu wajitokeze kwa wingi ili kuhakikisha wanapata burudani ya aina yake na pia kutakuwa n zawadi mbalimbali kwa watazamaji'' Amesema Bi Bhoke.

Aidha makundi matano yatakayopatikana kesho yataanza mazoezi pamoja na makundi mengine 10 ya usaili wa kwanza na wa pili katika kusaka mshindi wa nafasi ya robo fainali, nusu fainali na fainali yenyewe.

Shindano hili linaoneshwa na EATV kila siku ya Jumapili kuanzia saa moja kamili jioni kwa udhamini wa Vodacom na Coca-Cola.

Tags: