Alhamisi , 18th Jul , 2019

Msanii wa kike kutokea nchini Kenya Victoria Kimani, amemtupia dongo la lawama staa wa muziki wa RnB na Pop Duniani Beyonce "Queen B" kwa kosa la kuwatenga wasanii wa Kenya na wasanii wa Africa Mashariki.

Victoria Kimani (kushoto) na Beyonce.

Victoria Kimani ameeleza hayo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, baada ya kuona hakuna hata msanii mmoja wa Kenya na kutoka Africa Mashariki kuwepo kwenye Album yake mpya ya "The Lion King: The Gift", ambayo Album hiyo amewapa mashavu zaidi wasanii wanaotokea nchini Nigeria.

Victoria Kimani ali-tweet kwa kuandika "Filamu imebeba misingi ya nchi ya Kenya sawa, lakini Malkia wetu ametusahau sisi wa Kenya na wana Africa Mashariki, Sisi hatujawakilisha katika Album yake, inauma sanaa ni hivyo tu" ameandika Victoria Kimani.

Siku ya Jumanne ya Julai 16, Beyonce alitangaza kuachia Album yake mpya ambayo ndani ya Album hiyo ameshirikisha wasanii kutokea barani Africa ambao ni Wizkid, Tekno, Burna Boy, Mr Eazi, Yemi Alade, Tiwa Savage wote hawa wanatokea nchini Nigeria, pamoja na Shatta Wale kutokea nchini Ghana.