VIDEO : Kufuru ya Mjengo wa Alikiba Tabata

Jumatano , 22nd Jul , 2020

Msemaji Mkuu wa Wanawake kutoka East Africa TV na East Africa Radio Maryam Kitosi, amefanya ziara ya kumtembelea Mama mzazi wa staa wa BongoFleva Alikiba, Abdukiba, Zabibu Kiba na Abuu Kiba.

Ghorofa la msanii Alikiba Tabata

Mahojiano yamefanyika nyumbani kwa Alikiba Tabata Dar es Salaam, ambapo anamiliki ghorofa kubwa na kumfanya awe mmoja wa wasanii ambao wanamiliki mijengo mikubwa hapa nchini.

Kingine ni magari matatu ya kifahari anayoyamiliki msanii huyo pamoja na mbwa wadogo wadogo wawili maarufu kama vi-mbwa vya kudangia.

Zaidi tazama mjengo wake hapa chini kwenye video.