Vita yamuweka pabaya Pretty Kind

Alhamisi , 6th Dec , 2018

Muigizaji wa filamu bongo ambaye pia amejaribu kugeukia upande wa muziki, Pretty Kind, ameweka wazi sababu za yeye kubadilika kitabia na kuwa na tabia zisizofaa, licha ya kukua kwenye familia ambayo inafuata maadili ya dini.

Akizungumza na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Pretty Kind amesema kwamba yeye alizaliwa kwenye familia ya kidini isipokuwa vita iliyopo kati yake na shetani ndiyo iliyomsababishia yeye kujiingiza kwenye maisha ya anasa na kufanya mambo yasiyo faa kwenye jamii.

“Toka nimezaliwa nimekua kwenye maadili ya dini, sema majaribu ya shetani, kwa sababu kuna vita ambayo inatokea, unapokuwa kwenye familia yenye maadili ya dini kuna majaribu ambayo yanakuwa yanatokea, yanakurudisha nyuma, vita inakupiga ”, amesema Pretty Kind.

Akiendelea kuelezea suala hilo Pretty Kind amsema kwamba kwa sasa anamshukuru Mungu amembadilisha, na kwamba hawezi tena kufanya mambo yasiyofaa mbele ya jamii.