Jumamosi , 21st Sep , 2019

Staa wa muziki Ali Kiba ameeleza vituko anavyovikumbuka, wakati alipokuwa anasoma shule ya msingi Upanga Jijini Dar Es Salaam.

Alikiba

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital ameeleza,

"Kiukweli mimi nilikuwa mtundu sana, kila siku ya Ijumaa kwa sisi Waislamu tulikuwa tunapewa ruhusa ya kutoka mapema kwenda msikitini, lakini kuna siku tulikuwa na Mwalimu mmoja ambaye alituzuia kwenda kwa sababu hatukumalizia 'Home work' nakumbuka hiyo siku tulitoroka darasani kwa kupitia dirishani na kwenda kumdanganya mlinzi" ameeleza Ali Kiba.

Aidha Ali Kiba amesaidia kukarabati ujenzi wa madarasa wa shule hiyo na sehemu ya kuwekea uchafu pamoja na kupaka rangi baadhi ya madarasa yanayopatikana shuleni hapo.

Mchango huo wa kukarabati ujenzi umetokana na shirika la SamaKiba Foundation, akishirikana na mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya KRC Genk.