Jumanne , 8th Jul , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Walter Chilambo amesema kuwa kutokana na muziki unavyokwenda hivi sasa anategemea sana shoo mbalimbali kuliko utoaji albamu.

Msanii wa bongo Walter Chilambo

Msanii huyo aliyeibuliwa na shindano la kusaka vipaji vya kuimba nchini ametoa kauli hiyo wakati akielezea mpango wake wa kuachia traki yake mpya ya 'Fanya Haraka' ambayo imetoka rasmi hii leo.

Akiongea na eNewz Walter amesema wimbo huu ameufanyia kazi Tongwe Records chini ya prodyuza mkali Geof Master ambapo pia ameweka wazi kuwa mpaka sasa hajafikiria kutoa albam japokuwa ana nyimbo nyingi sana.

Huu utakuwa ni wimbo wake mpya wa tano kutoka zikiwemo za awali ambazo ni Siachi, Doro Doro, Mi ni wako pamoja na Mavela.

Pata kitu kipya kipya kabisa kutoka kwake Walter 'Fanya Haraka'.