"Wanawake sio dhaifu, nimeingia Labor" - Shetta

Jumatatu , 10th Aug , 2020

Msanii Shetta amefunguka kusema anaipinga kauli inayosema wanawake ni dhaifu kwa sababu amebahatika kuingia Leba wakati mkewe mama Qaylah alipojifungua mtoto wao wa pili na kushudia tabu alizopata wakati akiwa leba.

Msanii Shetta

Shetta amesema wanawake ni watu ambao wanatakiwa kuheshimiwa sana kwa sababu kitendo cha kulea na kumleta kiumbe duniani ni kazi kubwa na inakuwa nusu kifo kutokana na maumivu na shida ambazo anapata wakati anajifungua.

"Nilimuona mke wangu Mama Qaylah wakati yupo leba anajifungua mtoto wetu wapili, nafikiri wanawake ni watu amabo wanatakiwa tuwaheshimu sana, kwa sababu kitendo cha kubeba ujauzito miezi 9, ile hali ya kujifungua inakuaga ni nusu kifo na kazi kubwa kabisa ni kitendo cha kulea watoto, sipendi kabisa kusikia mtu anasema mwanamke ni kiumbe dhaifu" ameeleza Shetta 

Zaidi tazama hapa chini kwenye Video.