Jumatano , 19th Oct , 2016

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye awali aliwahi kutamba na wimbo 'Sina Raha' amefunguka na kusema kwenye muziki wapo watu ambao wanatamani kuona akifeli katika muziki.

Sam wa Ukweli (wa pili kulia) akiwa Planet Bongo iliyokuwa ikiruka LIVE kutoka Banana DSM

Sam wa Ukweli alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho leo kilikuwa kinaruka moja kwa moja kutoka Ukonga Banana na kudai kuwa hakuamua yeye kukaa kimya kwenye muziki bali mkataba aliokuwa amesaini na uongozi wake wa awali ndiyo ulimpelekea yeye kukaa kimya kwani uongozi huo uliyumba kiuchumi na wakawa hawataki kumuachia kutokana na mkataba aliosaini.

"Wapo watu wanatamani mimi nifeli. Unajua hata ukimya wangu kwenye muziki ulitokana na 'Management' yangu ya pili, uongozi uliyumba kiuchumi na mkataba niliokuwa nimesaini ulikuwa unanizuia kufanya kazi na mtu mwingine na wao wakawa hawataki kuniachia hivyo ilinibidi nisubiri mpaka muda wa mkataba na wao uishe ili niwe huru na kazi, ndiyo kama hivi sasa nimemaliza muda huo ndiyo maana nimekuja na kazi yangu hii mpya 'Kisiki'" alisema Sam wa Ukweli

Mbali na hilo Sam wa Ukweli ameachia wimbo wake mpya ambao unafahamika kama 'Kisiki' ambao ndani yake amezungumzia mambo makuu matatu, Afya, Mapenzi na Pesa kwani yeye anasema hivi ni vitu vitatu vinavyoendana.