Jumatano , 19th Mei , 2021

Muziki wa Bongo Fleva bado utabaki katika ramani ya dunia kwa vizazi na vizazi kwani licha ya mafanikio yanayoendelea kuzungumzwa kila siku.

Pichani ni wasanii wa Bongo Fleva, Mr II (kushoto), Lady Jay Dee (katikati) na Professor Jay (kulia)

Ila tambua ni wazi itachukuwa muda mrefu kwa wasanii wa kizazi kipya kuvunja rekodi za baadhi ya wasanii wa zamani ambao wanamilikia album nyingi.

Miaka kadhaa iliyopita soko la album nchini lilidorola, hali ambayo ilisababisha wasanii wengi kuacha utamaduni huo na kukimbilia kuachia wimbo/nyimbo (single).

Kwa zamani album zilikuwa zikifanya vizuri sokoni kiasi kuwafanya wasanii kutoa album kwa wingi kuliko wimbo/nyimbo na ina aminika kuwa na album kwa msanii ndio utambulisho mzuri zaidi.

List ya wasanii wa 5 wenye albamu nyingi Bongo.

1.Mr II (Sugu).

Anatajwa kuwa Rapper wa mwanzoni kabisa kwenye kiwanda cha Bongo Fleva, aliyeanza muziki kipindi cha miaka ya 90’s na kutamba na ngoma yake “Wananiita Sugu”, pioneer huyu alifanikiwa kurekodi na kuachia album 10 ambazo; Ni Mimi (1995), Ndani ya Bongo (1996),Niite Mister II (1998), Nje ya Bongo (1999), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001), Itikadi (2002), Sugu (2004), Coming of Age-Ujio Wa Umri(2006) na VETO (2009).

2.Lady Jay Dee.

Ni Commando haswa, Binti Machozi ambaye mawimbi yake ya sauti yalifanikiwa kuwa chachu kwa wasanii wengi wa kike Tanzania leo anajivunia kuwa miongoni mwa wasanii wenye album kibao, anazo 8 ambazo ni;Machozi (2000), Binti (2003), Moto (2005), Shukrani (2007), Ya 5. The Best of Lady Jaydee (2012), Nothing But The Truth (2013), Woman (2017) na 20 The Album (2021).

3.Professor Jay

Alibadilisha upepo wa game, alifanikiwa kufanya muziki ambao uliwateka mpaka wazee ambao awali walikuwa wakiamini sanaa ni uhuni.

Ngoma kama Nikusaidiaje na Ndio Mzee zilimpa heshima na kuuheshimisha muziki wa Bongo, ana album 6 ambazo ni; Machozi Jasho na Damu (2001), Mapinduzi Halisi (2003), J.O.S.E.P.H (2006), Aluta Continua (2007), Izack mangesho (2014) na Kazi Kazi (2016) huku album ya 7 ikiwa ipo njiani.

4.Soggy Dog

Inahisiwa kuwa ndiye mwanamuziki wa kwanza Tanzania kuanza kuimba akiwa na umri mdogo zaidi kwa kipindi hicho akiwa shule mwaka 1993, mpaka sasa ana album 5; Bongo Newyork (1999), Tuko Pamoja (2000), Niite Chief Rumanyika (2004), Machi 11 (2006), na Ilala.

5.Juma Nature.

Muite Sir. Nature, huyu ni ng’ombe asiyezeeka maini, tangu aingie rasmi kwenye game kila kizazi kinaliimba jina lake, ni legendary ambaye ana album 5 ambazo ni;    Nini Chanzo (2001), Ugali (2003), Ubinadamu-Kazi (2005), Zote History (2006) na Tugawane Umaskini (2009).