Jumatatu , 4th Feb , 2019

Msanii wa kike asiyeishiwa drama kutoka kiwanda cha Bongo Muvi, Wema Sepetu ameibua jipya kuhusiana na ishu yake ya kupungua uzito ambapo amesema sababu hasa iliyomfanya awe hivyo ni msongo wa mawazo ‘stress’.

Kulia ni Wema Sepetu wakati akiwa mnene, na kulia ni Wema Sepetu wa sasa ambaye amepungua kwa muda mfupi.

Wema kwa mara ya kwanza amesema kuwa hajawahi kukata utumbo ili apungue kama watu wanavyodai, isipokuwa kipindi alichopitia kwenye lile sakata la kuvuja kwa picha zake za chumbani na Patric Christopher ‘PCK’ kilikuwa kigumu mno kwani alikuwa anapitisha hata siku tatu bila kula chochote mpaka anapepesuka.

Watu nawashangaa sana, wanaona kukatwa utumbo ni kitu rahisi ee? Mimi nimekon­da kwa sababu ya mawazo makali niliyokuwa nayo na si vitu vingine maana nilikuwa kwenye wakati mgumu sana", amesema Wema.

Wema ameongeza kuwa, "Yaani hujui tu ninavyoufura­hia huu mwili wangu wa sasa, nimekuwa sio mzito tena na navaa nguo ambazo nataka na napendeza zaidi tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, kwa kifupi najipenda hivi nilivyo".