Jumanne , 17th Feb , 2015

Star wa michano Young Killer, akiwa moja ya wasanii ambao wamekwishafanya ngoma kadhaa kuwakilisha matatizo yanayoikumba jamii, amesema kuwa mara nyingi msanii anapofanya hivyo anatumia nafasi yake vizuri kuiwakilisha hali halisi ya jamii husika.

Young Killer

Amesema huo kama wajibu wake na sio kuangalia faida.

Young Killer ambaye leo hii anaachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina Utusamehe akishirikiana na Young Dee, amesema kuwa kazi za namna hiyo zinamuweka msanii kama mtetezi wa watu wasiokuwa na sauti mitaani, licha ya mabadiliko katika soko la muziki sasa ambalo huvuta rekodi za burudani pekee.