Yusuph Mlela aeleza tabia ya kukopa kwa wasanii

Jumatatu , 4th Nov , 2019

Msanii wa filamu nchini Tanzania Yusuph Mlela, ameieleza EATV & EA Radio Digital juu ya suala zima la wasanii wa Bongo Movie kupenda kupendeza na kula bata ila mara nyingi wanaishia kukopa.

Pichani ni msanii wa filamu Yusuph Mlela

Kwa upande wake Yusuph Mlela, amesema labda tabia hiyo ipo kwa wasanii wengine ila kwake anapenda ale kile anachokipata na kuridhika hata kama ni kidogo.

"Labda watu wanasema kwa wasanii wengine ila mimi binafsi sikopi kopi, napenda nile kile ninachokipata na naridhika nacho hata kama ni kidogo nitajua nakigawa vipi  hata nikipata kikubwa najua nitagawanya vipi, lakini kwenye maisha yangu suala la kukopa huwezi kusikia kashfa hizo" amesema Yusuph Mlela. 

"Siogopi kudaiwa lakini naamini kabisa ninachokipata naweza ku-balance kikanifanya nikaishi vizuri na nikapendeza kama hivi ninavyoonekana na hayo mambo yanasemekana yapo ila kwangu mimi sijawahi kukutana nazo sana" ameongeza.