Msuva amkaribisha Thomas Ulimwengu Jangwani

Alhamisi , 17th Nov , 2016

Mshambuliaji Saimon Msuva wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, kwa mara ya kwanza amezungumzia taarifa za Thomas Ulimwengu kuichezea timu hiyo.

Thomas Ulimwengu

Akijibu maswali ya mashabiki wa soka kwenye kipindi cha KIKAANGONI kupitia Facebook East Africa Television, Msuva amesema iwapo Thomas Ulimwengu atakuja kucheza timu ya Yanga, itakuwa ni jambo zuri kwao kwani Ulimwengu ana uzoefu mkubwa, hivyo watajifunza kitu.

"Sijajua kama kweli atakuja, kama atakuja itakuwa vizuri kwetu, Thomas Ulimwengu atatupa changamoto kwa sababu kuna vitu vingi amejifunza huko Mazembe alikokuwa, hivyo itakuwa changamoto kubwa kwetu na kwa timu pia", alisema Saimon msuva.

Saimon Msuva, akiwa Kikaangoni