Afurahia kufanya kazi na maiti kwa miaka 32

Jumatatu , 3rd Jun , 2019

Basil Enatu (57) ambaye ni mhudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Soroti chini Uganda, amesema kuwa anafurahi sana kufanya kazi na maiti kwa takribani miaka 32.

Basil Enatu.

Akiongea na Daily Monitor, mzee Enatu anasema huwa ni raha sana kufanya kazi na maiti kwani hawasumbui na wamekuwa marafiki wakubwa kwake.

Napenda kufanya kazi na waliofariki kwani maiti  hawasumbui kabisa tofauti na watu walio hai”, amesema Enatu.

Enatu ajira yake ni kuwaosha na kuwavisha maiti na wakati mwingine madaktari pia humtaka awasaidie kuvikata vipande vya mwili wakati wa upasuaji wakati mwili unafanyiwa uchunguzi.

Mzee Enatu baba wa watoto kumi na wawili licha kuipenda kazi yake amesema ina changamoto kwani wengi hukataa hata kumsalimia wakihofia mikono yake.