Agundua kuishi bila sehemu za siri kwa miaka 17

Jumanne , 7th Jan , 2020

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Julian Peters (29), amesema aligundua anaishi bila kuwa na mfumo wa uzazi wa mwanamke, wakati akiwa na umri wa miaka 17.

Picha ya mwanamke huyo asiyekuwa na sehemu za uzazi

Mwanamke huyo amesema anaishi bila ya uke, kizazi na mfuko wa uzazi kama walivyo wanawake wengine na ameshahangaika katika hospitali ili kutatua tatizo hilo ila kwa bahati mbaya ameambiwa amezaliwa hivyo bila ya kuwa na mfumo wa uzazi wa mwanamke.

Julian Peters amesema ameelewa na amekubaliana na hali hiyo, japokuwa jamii hufikiria vibaya na kuhusisha jambo hilo na imani za kishirikina au kutuhumiwa tatizo hilo limekuja baada ya kutoa mimba.

Akizungumzia suala la mahusiano na hali yake ilivyo amesema  "Kwa hali yangu, nipo tayari kwa chochote na nipo tayari kuwa na yeyote atakayetaka, pia kwa yeyote atayetaka kuondoka kuwa kwenye mahusiano na mimi namuacha aende."

Aidha Julian Peters amewashauri wanawake wengine, wenye hali kama yake kwa kusema wajipende wenyewe na wajue kama Mungu anawapenda sana, na jamii isiwalazimishe kujua kitu gani kilichowakuta kwenye maisha yao.

Source Tuko News.