Aolewa kwa milioni 20, Ng'ombe 520 na gari tatu

Jumapili , 11th Nov , 2018

Hatimaye familia ya mrembo wa Sudan ya Kusini aliyekuwa anagombewa na wanaume wengi walioahidi kutoa mahali kubwa zisizo za kawaida, ameolewa kwa mahari ya ng’ombe 520 na magari matatu aina ya Toyota V8.

Nyalong Ngong Deng, akiwa na mume wake Kok Alat.

Mrembo huyo, Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka, ambapo kila mmoja alikuwa tayari kutoa mahali kubwa ikiwa ni pamoja na shilingi milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za Tanzania.

Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita, Novemba 9, binti huyo wa kabila la Dinka aliibua mshangao kwa watu waliokuwa katika sherehe hiyo.

Kulingana na utamaduni wa Dinka na Nuer, bei ya mahari kwa kawaida ni ng'ombe 20 hadi 40 hivyo binti huyo amendika historia ya pekee katika kabila lake kwa kuolewa kwa mahari ya ng'ombe 520 na vitu vingine vya thamani.