Utafiti mpya uliofanywa na mtandao wa masuala ya harusi wa ''The Knot'' umebaini kuwa takribani 90% ya wanaume kwa sasa wako tayari kufanya sherehe ndogo ya harusi (Small Wedding) au hata kuacha kabisa kuliko kufanya sherehe kubwa
Sababu kubwa iliyotajwa ni Uchumi, huku Wanaume wengi wameeleza kuwa wanapendelea kuepuka gharama kubwa za kumbi, vyakula, watu wengi na badala yake fedha hizo zitumike kama mtaji wa maisha yao ya baadaye.
Hapa kwetu sasa mambo ya ''ngoja nifunge mtaa leo'' au kauli ya ''nimechanga kwenye sherehe nyingi sana wacha na mimi wanichangie'' lakini wanaume wengi kwa sasa wanasema "Hapana, tufikirie kwanza maisha baada ya harusi''



