Atolewa kwenye ndege kisa kuiombea ipate ajali

Jumanne , 12th Mar , 2019

Mwanaume mmoja ametolewa kutoka kwenye ndege moja iliyokuwa ikisafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Islamabad nchini Pakistan kwenda Dubai, baada ya kufanya maombi akimuomba ‘mungu wake’ kusababisha ajali ya ndege hiyo.

Abiria huyo ambaye alitambuliwa kwa jina moja la Khalil alikuwa akisafiri kuelekea Australia kupitia Dubai, na imefahamika kuwa alianza kuomba maafa ya mauti yatokee punde tu alipoketi ndani ya ndege hiyo katika Uwanja wa Ndege.

Maombi yake yaliwafanya abiria kuhofia na kuanza kuingiwa na wasiwasi, hasa wasafiri na wahudumu wa ndege waliokuwapo.

Baada ya tukio hilo Rubani alitahadharisha idara ya ulinzi katika uwanja huo , na maafisa wa usalama walipofika wakamuondoa ndani ya ndege.

 

Source

Daily Mail UK