Jumanne , 19th Sep , 2023

Kijana wa miaka 15 kutokea nchini India anayefahamika kwa jina la Sidakdeep Singh hakuwahi kunyoa nywele zake tangu azaliwe na sasa hivi anashikilia rekodi ya kijana wa kiume mwenye nywele ndefu Duniani kwa mujibu wa Guinesss World Records

Sidakdeep Singh Chahal

Nywele zake zina urefu wa sentimita 146 sawa na futi 4. Sidak hakuwahi kukata nywele kwa sababu ya utamaduni wa dini yake ya Sikh, ambapo hawaruhisi kukata nywele hata moja na wanaamini ni zawadi kutoka kwa Mungu.

Kwa mara ya mwisho rekodi hii ilikuwa inashikiliwa na Nilanshi Patel kutokea nchini India pia, ambaye nywele zake zilikuwa na urefu wa sentimita 200 sawa na futi 6, alizikata nywele zake mwaka 2021 na kuzipeleka makumbusho.