Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Ifahamu tamaduni hii ya kupasua midomo

Ijumaa , 12th Oct , 2018

Jamii moja katika kisiwa cha Phuket  kusini mwa Thailand imeendesha tamasha la kitamaduni na la kidini linalojulikana kwa jina la ‘Taoist’ kwaajili ya kujitakatisha dhidi ya madhambi, ambapo washiriki husheherekea kwa kujichoma mishale, visu  na mapanga katika mashavu yao.

Tamasha hilo lenye asili ya China hufanyika mwezi Oktoba kila mwaka, ambapo tamasha la mwaka huu limefanyika kuanzia 9, Oktoba likihudhuriwa na jamii kubwa ya Wachina wanaoishi katika eneo hilo .

Moja ya matukio ambayo hufanyika katika tamasha hilo ni pale ambapo mtu mmoja hujichoma visu vingi vikali katika mashavu yake na mwingine hushikilia kichwa chake na kukata ulimi wa mtu huyo kwa kutumia shoka, na kumwacha akibubujikwa na damu kifuani.

Watu hao waliokatwa vitu vikali ni miungu ambao hutembea ardhini wakionesha miujiza yao pamoja na vipande vya nyama vilivyokatwa, ili madhambi ya watu wao yasafishwe”, amesema Pathompong Reanthong, ambaye ni mmoja ya waandaaji.

Malengo ya sherehe hii ni kwaajili ya watu kuona imani zao, na kujiepusha na matumizi ya nyama. Ni sherehe ya kuondoa mambo mabaya ”, ameongeza.

Washiriki wa sherehe hiyo hawaruhusiwi kula nyama wakati wa mashindano. Kwa mujibu wa washiriki, sherehe hiyo huwakumbusha mwaka 1825 ambapo wageni wa kwanza raia wa China katika eneo hilo walipitia matukio hayo.

Jamii hiyo inaamini katika milo ya mboga za majani na matunda, ikiwa ni katika namna ya kuboresha afya zao.

Kupita juu ya makaa ya moto ni njia ya mwisho kabisa kwa washiriki wa tamasha hilo, tukio ambalo ndilo linalotarajia kuhusisha maelfu ya watu.

HABARI ZAIDI

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton

Maduka ya Wafanyabiashara yakiwa yamefungwa

Wamiliki wa maduka Mebya wafunga biashara zao

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu