Jumanne , 31st Mei , 2022

Meneja Rasilimali watu wa ITV na Radio One, Bi. Hellen Elipokea amekabidhi taulo za kike kupitia kampeni ya Namthamini katika ofisi za East Africa TV & Radio kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ITV na Radio One.

Bi. Hellen akikabidhi taulo za kike katika ofisi za East Africa TV & Radio

Idadi ya taulo za kike zilizotolewa zitaweza kusaidia watoto wa kike 50 kuendelea kubaki shuleni kwa mwaka mzima bila kikwazo cha kukosa masomo kutokana na ukosefu wa taulo za kike.

"Huu ni mchango wa ITV kuwaunga mkono East Africa TV na East Africa Radio, tunaomba kila anayeona shughuli hii naye ajaribu kuwachangia ili kuwaunga mkono kwa kazi mnayofanya kumsaidia msichana wa Tanzania'' - Bi. Hellen Elipokea