Jamaa apiga pesa kisa kujifananisha na Mo Salah

Ijumaa , 18th Oct , 2019

Unapoambiwa binadamu wapo wawili wawili, usishanagae maana hii imetokea huko Kaskazini mwa bara la Africa nchini Misri, kuna jamaa anaitwa Ahmed Bahaa ambaye amefanana sawa sawa na mchezaji wa Taifa hilo na klabu ya Liverpool, Mohammed Salah.

Jamaa huyo ambaye pia ni Mhandisi, amekiri kuwa ameshafanya matangazo mengi kama ya simu, vinywaji na kampeni za madawa ya kulevya ili kujipatia pesa kwa kujifanyisha Mohammed Salah.

Wakati anafanyiwa mahojiano katika kituo cha habari cha Al Nahar TV, Ahmed Bahaa amesema.

Nimefanya matangazo mengi na Salah, Salah kwa kweli hawezi kukaa na kufanya tangazo moja kwa muda mrefu, ninachukua muda mwingi kurekodi matangazo hapa na nitaenda pia Uingereza kumalizia kurekodi naye Salah, hii ni kuharakisha mambo kwa sababu yeye hana muda mwingi wa kufanya matangazo” amesema Bahaa. 

Baada ya kumaliza kufanya mahojiano hayo watu wengi walishangaa kuona muonekano wake wa kweli kama Mohammed Salah mwenyewe na wengine walitumia nafasi hiyo kusambaza picha zake na video zake mitandaoni.