Ijumaa , 6th Sep , 2019

Jogoo mmoja aliyejulikana kwa jina la Maurice mwenye miaka minne, ameshinda kesi iliyokuwa inamkabili nchini Ufaransa.

Jogoo

Jogoo huyo alikuwa anashtakiwa na majirani zake kwa kuleta shida na usumbufu wa kupiga kelele, wakati wa asubuhi huku wakitaka wahame katika maeneo waliopo.

Mahakama imeamuru Jogoo huyo alipwe fidia ya Euro 1,103 sawa na shilingi Milioni 2 za kitanzania kama usumbufu, ambao ulisababishwa kutoka kwa majirani ambao walianza kumshtaki kuanzia mwaka 2017.

Mwanasheria wa Jogoo Maurice amesema, Kuku ni ndege asiye na hatia ni jambo la kipuuzi kuona watu wanamshtaki kutokana na alivyofanya.

Aidha mmiliki wa Jogoo huyo amesema ushindi wa kesi alioupata dhidi ya Jogoo wake ni ushindi wa kila mtu, na atakuwa ni mfano wa viumbe wengine duniani kote.

Pia uongozi wa juu nchini Ufaransa umesema viumbe kama Jogoo wanatakiwa wapewe heshima na wawekwe katika nyumba ya makumbusho kwani anawakilisha nembo ya taifa lao.

Wanyama na wadudu wengine walioshtakiwa kuhusu suala la kupiga kelele nchini Ufaransa ni Mbuzi, Ng'ombe, Nzige (balale) pamoja na kengele ya kanisani.