Jumapili , 15th Mei , 2022

Siku ya leo usiku na kesho Mei 16 huenda likatokea tukio la kupatwa kwa mwezi kwa mujibu wa utafiti wa NASA, ambapo mwezi utakua karibu na Dunia na utaonekana kwa ukubwa zaidi ukiwa na rangi nyekundu.

Tukio hilo linatabiriwa litatokea tena Novemba 8 mwaka huu.

Tovuti ya timeanddate.com imeandika tukio hilo litaonekana vizuri katika baadhi ya sehemu Duniani ambapo bara la Ulaya litaoneka kwa nchi za magharibi, bara la Marekani kaskazini, na Afrika. 

 

katika mji wa Dar es salaam tukio hilo litatokea saa 10:32 alfajiri na saa 11:27 alfajiri.