Maye Musk katika jarida la 'Sports Illustrated Swimsuit'
Maye Musk amekuwa mwanamitindo mzee kuwahi kutokea katika jarida la 'Sports Illustrated Swimsuit' akichuana na Kim Kardashian na Ciara ambao pia wametokea katika jarida hilo kwa mwaka 2022.
Maye amefanya kazi hiyo kwa miaka 50 na hata kabla ya kumzaa Elon Musk, na alishawahi kutokea katika majarida makubwa kama Vogue.