Mastaa waililia Afrika Kusini

Jumanne , 3rd Sep , 2019

Nchini Afrika Kusini kuna machafuko na vurugu ambazo zinaendelea kutoka kwa wenyeji ambao wanachochea suala la ubaguzi wa rangi kwa kuwapiga, kuwaibia na kuwachoma moto wageni na raia ambao sio wa nchi hiyo.

Wasanii na watu maarufu

Afrika Kusini ina idadi ya wageni na wahamiaji wapatao milioni 2.3, kutokea mataifa mbalimbali ikiwemo China, India, Marekani na watu wa mashariki ya kati kutokea bara la Ulaya.

Hii ni orodha ya mastaa ambao wameandika kupitia mitandao ya kijamii kwa kuonyesha kuguswa, kutokana na hali inayoendelea nchini humo.

Nikki wa Pili "Kinachotokea SA ni moja ya sifa ya kizazi cha sasa ni mihemko na kutokuwepo na fursa kubwa ya kujielemisha. Moja ya sifa kubwa ya babu zetu wakati wa utumwa au ukoloni kina Malcom X, Samora, Mwalim ilikua ni kujielimisha na kupambana kujifunza".

Skales  "Mnasema wageni wamekuja kuchukua kazi zenu, Wanawake wenu, Wanaleta uhalifu kwenu. Ila nyinyi Waafrika kusini ndiyo mnawaua, mnawakaba, na kuwabaka kila siku".

Zari The Bosslady  "Nanyoosha mikono yangu juu, wenyeji wanafanya mambo ya kibaguzi kwa kuwashambulia wenyeji kwa kuwapiga kuwaibia. Kemea Ubuguzi wa rangi".

Rosa Ree  "Mandela amka uone wanao wanavyofanya kwenye nchi uliyoteseka na kuipigania, ni muda halali wa Yesu kurudi kutusaidia, Eh Mwenyezi Mungu tusamehe kwani hatujui tuyafanyayo".

Yemi Alade "Inatosha sasa hali hii itaanedelea hadi lini, Africa ndiyo nyumbani kwetu, tunatakiwa kuitwa umoja wa mataifa ya Africa hatuitaji kuona umwagaji wa damu tena".