Mazoezi huongeza nguvu za kiume

Jumatano , 4th Sep , 2019

Kwa mujibu wa tafiti kadhaa zimeonesha kufanya mazoezi angalau nusu saa mara tatu kwa wiki kwa mwanaume, husaidia kuongeza nguvu za kiume.

Mtu akifanya mazoezi

Utafiti uliofanyika mwaka 2016 kwa wanaume 261 ulionesha mafanikio makubwa kwa wanaume wote hasa baada ya kufanyishwa mazoezi kwa muda kadhaa ndani ya wiki.

Timu ya uchunguzi ilichofanya kwa watu wote 261 walifanyiwa majaribio katika maeneo yote mawili, kwanza ni kwa kufanyishwa mazoezi mara kwa mara kwa wiki kadhaa na baadaye kuachishwa kufanyishwa mazoezi.

Matokeo yalionesha kipindi wakiwa wanafanyishwa mazoezi afya yao kwa upande wa njia za uzazi ziliimarika zaidi ikiambatana na kuongezeka kwa ubora wa mbegu za kiume kwa kipindi ambacho walikuwa wakifanya mazoezi tofauti na kipindi ambacho walikuwa hawafanyi mazoezi.

Lakini wataalamu wanashauri pia ufanyaji wa mazoezi kwa kiasi kikubwa unaweza kupelekea matatizo ya nguvu za kiume, hivyo yakupasa kuwa na kiasi pale unapofanya mazoezi kwenda na muda sahihi kila mara unapofanya mazoezi.

Kiongozi wa utafiti huo bwana Behzad Hajizadeh Maleki, alifafanua zaidi kuwa licha ya utafiti huo kuonesha kusaidia kuongeza ubora wa mbegu za kiume na faida nyingine, katika njia za uzazi kwa ishu ya wanaume ambao hawawezi kusababisha mimba sababu huwa sio ubora wa mbegu tu bali hutokana na sababu nyingine nyingi.

"Matatizo ya nguvu za kiume huwa yanachanganya hivyo kubadilisha mtindo wa maisha hayawezi kutibu tatizo hili kwa haraka," alisema.