Jumatatu , 5th Jul , 2021

Mchekeshaji MC Mboneke aliyejizolea umaarufu hivi karibuni kupitia vichekesho vyake vya irudiwe irudiwe, amesema kuwa endapo Mungu atampa kibali cha kufungua kanisa basi atafanya hivyo.

Mchekeshaji MC Mboneke

MC Mboneke ametoa kauli hiyo hivi karibuni kupitia kipindi cha MadiniDotCom cha East Africa Radio, kinachoruka kila Jumamosi kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 10:00 jioni na Grayson Gideon.

"Mungu akisema sasa Mboneke nataka nikufanye uwe kama Daudi na wewe ukaita watu ukawa-organise muwe mnalisema neno la Mungu ili watu wampokee, na mimi nita-appreciate nitasema asante Mungu," amesema MC Mboneke.